Waasi wa Syria wasalimu amri watarajiwa kuondoka Ghouta

Waasi wa Syria wasalimu amri watarajiwa kuondoka Ghouta

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema watu 105,000 wameondoka eneo linaloshikiliwa na waasi la Ghouta Mashariki

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema watu 105,000 wameondoka eneo linaloshikiliwa na waasi la Ghouta Mashariki wakiwamo 700 ambao wameondoka leo, tangu serikali ilipoanza mashambulizi ya kulikomboa eneo hilo mwezi mmoja uliopita. Shirika la habari la Urusi, RIA limeripoti hayo na kulinukuu jeshi, huku likirejelea shughuli ya kuwaondoa raia wakati wa vipindi vya usitishwaji mashambulizi kwa ajili ya kuwezesha huduma za kibinadamu. Rais wa Urusi, Vladimir Putin ambaye ni mshirika mkuu wa Rais wa Syria, Bashar al-Assad aliamuru usitishwaji wa mashambulizi kwa muda wa saa tano kila siku na kubuniwa kwa njia ambayo misaada ya kibinadamu inaweza kupitishwa na raia kuondoka Ghouta Mashariki. Wakati huo huo, shirika la habari linalomikiwa na serikali ya Syria limeripoti kuwa watu 7,000 wa familia za wanachama wa kundi la waasi wanajiandaa kuondoka Ghouta Mashariki karibu na Damascus ili kuelekea eneo la Kaskazini linaloshikiliwa na waasi.

Mwisho wa habari / 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky