Wairaq elfu 17 warudi katika makazi yao katika mkoa wa Nineveh

Wairaq elfu 17 warudi katika makazi yao katika mkoa wa Nineveh

Wizara ya mambo ya wahajiri nchini Iraq imetangaza kurudi kwa Wairaq elfu 17 katika maeneo yao waliokuwa wamekimbia katika mkoa wa Nineveh nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: wizara ya mambo ya wahajiri nchini Iraq imetangaza kurejea kwa Wairaq elfu 17 katika makazi yao ya zamani katika mkoa wa Nineveh.
“Jasim Muhamm” waziri wa mambo ya wahajiri nchini Iraq, amebainisha kuwa ofissi ya wizara ya mambo ya wahajiri nchini Iraq katika miji ya Al-Hamdaniayah, Bartalah, Baashiqah na Annemrud katika sehemu hizo wamerudi wananchi elfu 17 waliokuwa wamekimbia makazi yao, ofisi za wizara hiyo katika sehemu hizo ziliwapokea watu hao, huku wakisisitiza kuwa idadi hiyo ni chache zaidi ukilinganisha na waliokimbia ambao waliokuwa wakiishi sehemu hiyo,
Aidha wamebainisha kuwa kurudi kwa idadi hiyo ni kiashirio chema kinachoashiria kuwa ni mwanzo wa kurudi wananchi wengine walikuwa wamekimbia katika sehemu mbalimbali ya Iraq.
Kiongozi huyo alieleza kuwa idara yake imejipanga ipasavyo katika kutoa misaada mbalimbali kwa wananchi ambao wameanza kurejea katika makazi yao katika mikoa yote nchini humo.
Habari ziliotufikia zinaeleza kwamba, jumuia ya umoja wa Mataifa imeeleza kuwa wananchi wa Iraq wa waliohama na kuacha makazi yao nchini Iraq walifikia watu zaidi ya milioni tatu toka kuanza hujuma za kigaidi nchini humu mpaka sasa, ambapo walianza kuacha makazi yao toka mwaka 2014 zilipoanza hujuma za kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini humo na kushadidi zaid mwaka 2015 muda ambao kikundi cha kigaidi cha Daesh kiliiteka mikoa 6 ya Iraq.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky