Wajerumani 150 wa kikundi cha Daesh wauliwa nchini Iraq na Syria

 Wajerumani 150 wa kikundi cha Daesh wauliwa nchini Iraq na Syria

Hayo yametangazwa shirika la habari la Ujerumani kuwa wananchi wake 150 waliokuwa katika kikundi cha kigaidi cha wamepoteza maisha nchini Iraq na Syria

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: shirika la habari la Ujerumani usiku wa Alhamisi limetangaza kuwa: wananchi 150 wa Ujerumani waliungana na vikundi vya kigaidi nchini Iraq na Syria wamepoteza maisha nchini Iraq na Syria.
Watu elfu tano kutoka mataifa ya Ulaya walijiunga na kikundi cha kigaidi cha Daesh, baada tu ya kuundwa kikundi hicho mnamo mwaka 2014.
Shirika la habari la Ujerumani limeongeza kutangaza kuwa: baada ya kikundi cha kigaidi cha Daesh kusambaratishwa nchini Iraq na Syria, maelfu ya magaidi hao wamekuwa wakirudi katika mataifa yao, ikiwemu watu elfu na miambili wamerudi nchini Ufaransa na watu 970 wamerejea nchini Ujerumani.
Kwa mujibu wa ripoti hii, watu elfu 10 waliokuwa na itikadi ya kigaidi ya Salafia wanaishi nchini Ujeruni wakiwa raia wa nchi hiyo, ambapo katika hao watu 700 ni ambao tayari wanafungamano na vikundi hatari vya kigaidi, ambapo pia nitishio la usalama wa taifa hilo.
Shirika hilo lilimalizia kwakusema kuwa: kurudi kwa watu hao nchini Ujerumani na kuwepo kwa idadi kubwa ya masalafia nchini humo ni katika changamoto kubwa ambazo ni tishio la usalama wa taifa hilo.   
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky