Wakimbizi 31 wa Somalia wauwawa kufuatia shambulizi la ndege za Saudi Arabia + picha

Wakimbizi 31 wa Somalia wauwawa kufuatia shambulizi la ndege za Saudi Arabia + picha

Tukio hilo limetokea baada ya ndege ya Saudi Arabia kuushambulia mtumbwi wa wakimbizi wa kisomalia uliokuwa ukipita karibu na fukwe za Yemen na kusababisha kuuwawa watu 31 katika shambulio hilo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: baada ya majeshi ya Saudi Arabia kushindwa kukabiliana na majeshi ya Yemen, wameanza kufanya matukio kama hayo ya kuushambulia wasafiri wanaopita katika maeneo ya nchi ya Yemen.
Siku ya Alhamisi ndege aina ya Helikopta ya umoja wa majeshi ya kivamizi ya Saudi Arabia ilishambulia mtubwi wa wakimbizi wa Soamlia katika fukwe ya magharibi mwa Yemen, ambapo watu 31 wamekufa miongoni mwa watuy 80 waliokuwa katika mtumbwi huo.
Shirika la habari la Reuters katika habari hii limetangaza kuwa, mwanajeshi mmoja wa majeshi ya Yemen aliyekuwa katika sehemu ya Alhadidi ambayo iko chini ya kikundi cha Ansarullah nchini humo, baada ya kutangazwa kwa habari hii amesema kuwa: Helikopta ya Saudi Arabia ndio aliofanya shambulio hilo dhidi ya wakimbizi hao.
Kwa mujibu wa maelezo ya mmoja kati ya vikosi vya ulinzi vya fukwe za Yemen amesema kuwa, wakimbizi waliokuwa wameshambuliwa, walikuwa na vielelezo rasmi vya jumuia ya kusimamia wakimbizi ya kimataifa, ambapo walikuwa wakipita nchini Yemen kwenda nchini Sudani, ambapo walipofika karibu na mlango wa Bab-el-Mandeb ndipo wakashambuliwa na Helikopta ya kivamizi ya Saudi Arabia na kupelekea kuuwawa watu 31.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky