Wakurdi kushirikiana na jeshi la serikali dhidi ya Uturuki

Wakurdi kushirikiana na jeshi la serikali dhidi ya Uturuki

Vikosi vya wanamgambo wa kikurdi wa Syria na vile vya serikali ya Bashar asad vimekubaliana kwa jeshi la Syria kuingia katika mkoa wa Afrin ili kuwasaidia kupambana na uvamizi na mashambulizi ya Uturuki.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Vikosi vya wanamgambo wa kikurdi wa Syria na vile vya serikali ya Bashar asad vimekubaliana kwa jeshi la Syria kuingia katika mkoa wa Afrin ili kuwasaidia kupambana na uvamizi na mashambulizi ya Uturuki.

Mshauri wa utawala unaongozwa na wakurdi katika eneo la kaskazini mwa Syria Badran Jia Kurd, amesema kwamba vikosi vya jeshi vitasambazwa katika maeneo ya mpakani na vinaweza kuingia katika mkoa huo ndani ya siku mbili zijazo.

Mpango huo unapigia msumari vita inayozidi kuongezeka kaskazini mwa Syria, inayotokana na mtandao wa ushindani na ushirikiano miongoni mwa majeshi ya Kikurdi, serikali ya Syria, makundi ya waasi yaliyogawika, Uturuki, Marekani na Urusi.  Uhusiano mgumu baina ya serikali ya Damscus na vikosi vya jeshi la Kikurdi la Syria, ambayo kila mmoja anashikilia eneo zaidi dhidi ya upande mwingine katika vita, utakuwa na umuhimu namna mgogoro huo utakavyotatuliwa.

Ankara ilianzisha mashambulizi ya ardhini na angani katika mkoa wa Afrin mwezi uliopita ikawalenga wanamgambo wa wa kikurdi wa YPG, ambao inawachukulia kama kundi la kigaidi lenye mafungamano na kundi la waasi nchini Uturuki.

Marekani mshirika wa Uturuki katika jumuiya ya kujihami ya NATO imelipatia silaha kundi la YPG na kulifanya sehemu ya muungano wake inaouunga mkono nchini Syria dhidi ya serikali ya Syria. Lakini wakati ambapo Marekani ina majeshi yake katika maeneo mengi nchini Syria ambayo yanadhibitiwa na kundi la YPG na washirika wake upande wa mashariki, Marekani haijaliunga mkono kundi hilo katika mkoa wa Afrin.

Ingawa serikali ya rais Bashar al-Assad na kundi la YPG wamekuwa wakiepuka mgogoro wa moja kwa moja, mara kadhaa wamepambana na wana misimamo tofauti kuhusu mustakabali wa baadaye wa Syria. Wakati pande zote zikipendekeza makubaliano ya muda mrefu kuwa jambo linalowezekana, rais Assad anasema anataka kuidhibiti tena nchi zima.

Hayo yakijiri, Uturuki imesema kwamba haijawahi kutumia silaha zenye kemikali katika operesheni zake nchini Syria na inachukua tahadhari kubwa kuwajali raia, amesema waziri wa mambo ya nje Mevlut Cavusoglu akiyaita madai yaliyotolewa na vikosi vya wakurdi na makundi ya uangalizi kuwa "yasiyo na msingi" kwamba Uturuki ilifanya shambulio la gesi katika mkoa wa Afrin. Akiwa katika mkutano wa usalama mjini Munich, Cavusoglu alisema nchi yake itaendeleza mapambano dhidi ya kundi la YPG, akigusia pia ushirikiano na Marekani. "Tutaanza na Manbij. Baada ya YPG kuondoka hapa tunaweza kushirikiana na Marekani kutokana na uaminifu. Lakini kwanza YPG inahitaji kuondoka mara moja. Hii ni ahadi tuliyopewa na Marekani na tutazungumza namna gani ahadi hii itakavyotimizwa wakati wa majaribio ya kuanzishwa kwa taratibu baina ya nchi hizi mbili," alisema Mevlut.

Serikali ya Syria imewaruhusu baadhi ya wapiganaji wa Kikurdi, raia na wanasiasa kuingia Afrin kupitia eneo lake.

Mwisho wa habari / 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky