Walimu wawili wapelekwa mahakamani nchini Saudia kwa tuhuma ya kufanya ujasusi kwajili ya Iran

Walimu wawili wapelekwa mahakamani nchini Saudia kwa tuhuma ya kufanya ujasusi kwajili ya Iran

Walimu wawili nchini Saudi Arabia waliokuwa na umri wa miaka 39 na 41 wamepelekwa mahakamani na kuhukumiwa kwa kosa la kufanya ujasusi kwaajili ya Iran

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: walimu hao wawili nchini Saudi Arabia wamepelekwa mahakamani kwa tuhuma za kufanya ujasusi nchini humo kwaajili ya serikali ya Kiislamu ya Iran, ambapo wamehukumiwa na mahakama ya makosa ya jinai inayohusu masuala ya ugaidi na usalama wa taifa iliopo katika mji mkuu wa nchi hiyo Riyadh.
Walimu hao wawili wametuhumiwa kwa kosa la kutoa habari kwa Iran inayohusu bomba la mafuta liliopo baina ya mji wa “Baniq” na “Yanbau” ambapo urefu wa bomba hilo la mafuta ni kilometa 1200 na kila siku hupitisha pipa milioni tano ambazo hutoa katika Ghuba ya uajemi  kwenda maeneo mbalimbali.
Tuhuma nyingine zinazo wakabili ni kuwa wamepata mafunzo ya kuripua mabomba ya mafuta ambapo walijifunza katika kambi za kijeshi nchini Iran na Iraq, ili waje kufanya miripuko hiyo nchini Saudi Arabia.
Watuhumiwa hao waliokuwa na umri wa miaka 39 na mwingine 41, ni walimu wa shule za serikali ya Saudi Arabia, ambapo mahakama ya nchi hiyo wamewapa hukumu ya kunyongwa, huku wakipewa wiki  tatu ya kujipanga kwaajili ya kujitetea ukiisha muda huo.


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky