Wanajeshi 12 wa Sadia wauawa Yemen

 Wanajeshi 12 wa Sadia wauawa Yemen

Kiasi ya wanajeshi 12 wa saudi Arabia ambao wamekuwa wakifanya mashabulizi dhidi ya wayemen, wameuwawa katika mpaka wa kusini mwa nchi hiyo , kwa mujibu wa ripoti zisizo za kawaida zilizotolewa wakati nchi hiyo inafanya mashambulizi dhidi ya wananchi wa Yemen

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Kiasi ya wanajeshi 12 wa saudi Arabia ambao wamekuwa wakifanya mashabulizi dhidi ya wayemen, wameuwawa katika mpaka wa kusini mwa nchi hiyo , kwa mujibu wa ripoti zisizo za kawaida zilizotolewa wakati nchi hiyo inafanya mashambulizi dhidi ya wananchi wa  Yemen kwa lengo la kumrudisha madarakani rais Had ambaye wananchi wa Yemen wanampinga. Katika taarifa tofauti tangu Februari 5, Shirika la habari la Saudia SPA lilichapisha picha za mazishi ya kile ilichosema kuwa ni mashahidi , ambao limedai kuwa wameuwawa wakilinda mkapa wa kusini wa nchi hiyo. Ripoti ya hivi karibuni kabisa iliyochapishwa jana, imemtaja Jaber Haroubi kuwa mwanajeshi wa hivi karibuni kabisa kuuwawa. Shirika la habari la SPA pia limemnukuu baba wa mwanajeshi mwingine aliyeuwawa , Mohammed al-Manjahi , akisema anajivunia mwanae. Muungano wan chi 11 unaoongozwa na Saudi Arabia ukisaidiwa na Marekani ulianza mashambulizi ya anga dhidi ya Yemen Machi mwaka 2015 kuunga mkono serikali ya rais Abedrabbo Mansour Hadi ambayo inapingwa na wanachi wa Yemen kutokana na siasa zake za kibaguzi na kufuja mali za nchi hiyo masikini.

katika vita  hivyo Saudia arabia na washirika wake wameizingira Yemen tangu mwaka 2015 na kuzuia chakula na hata madawa na kusabisha janga la kitaifa, huku Umoja wa mataifa ukikaa kimya.

Mwisho wa habari/ 291  


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky