Wanajeshi 30 wauliwa kufuatia shambulio la kikundi cha kigaidi cha Bokoharam Nigeria

Wanajeshi 30 wauliwa kufuatia shambulio la kikundi cha kigaidi cha Bokoharam Nigeria

Kikundi cha kigaidi cha Bokoharam nchini Nigeria kimefanya mashambulizi ya kigaidi kaskazini mwa mashariki ya Nigeria katika mpaka na Niger na kupelekea kuawawa kwa wanajeshi 30 katika ya kambi za nchi hiyo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kikundi cha kigaidi cha Bokoharam kimeshambulia kambi moja iliopo kaskazini ya mashariki mwa Nigeria ambayo inapakana na nchi ya Niger nakupelekea kuuwawa wanajeshi 30 katika kambi hiyo.
Shambulio hilo limefanyika saa kumi alasiri ya leo kwa mida wa sehemu hiyo nakupelekea kuuwawa wanajeshi 30 na makumi ya wengine kujeruhiwa, ama idadi kamili ya waliojeruhiwa mpaka sasa bado hijafahamika.
Inasemekana kwa kikundi cha kigaidi Bokoharam ambachi ni katika vikundi vya kigaidi viliopo nchini Nigeria ambacho kilitanga kuunga mkono na kutoa kiapo cha utiifu kwa kikundi cha kigaidi cha Daesh, nacho kinaendelea kufanya mashambulizi ya kigaidi nchini humo huku kikidai kuwa kitatumia sheria ya Kiislamu katika taifa hilo.
Kikundi cha kigaidi cha Bokoharam kilianza mashambulizi yake nchini Nigeria mnamo mwaka 2010 ambapo mpaka sasa imepelekea kuuwawa kwa zaidi ya watu elfu 13 nchini humo, ambapo waathirika wakubwa wa mashmbulizi ya kikundi hicho ni watoto na wanawake.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky