Wanajeshi 4 wa Saudi Arabia wafa katika shambulio la majeshi ya Yemen

 Wanajeshi 4 wa Saudi Arabia wafa katika shambulio la majeshi ya Yemen

Vyombo vya habari vya Saudi Arabia vimethibitisha habari hizo kuwa wanajeshi wanne wa majeshi ya Saudi Arabia wameangamia kufuatia mapambano makali yaliotokea kati yao na majeshi ya Yemen kusini mwa nchi hiyo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: majeshi ya Yemen wamefanya shambulio kali dhidi ya safu za majeshi ya kivamizi ya Saudi Arabia na washirika wake.
Kwa mujibu wa taarifa hizi katika maeneo ya kusini mwa Yemen kumetokea mapigano makali kati ya majeshi ya Yemen na utawala wa uvamizi wa Saudi Arabia na washirika wake, ambapo kufuatia mashambulio hayo, wanajeshi wanne kutoka katika majeshi ya Saudi Arabia wamepoteza maisha.
Vyombo vya habari vya utawala wa Saudi Arabia umethibitisha habari hizo, ambapo kwa upande mwingine habari zinaeleza kuwa, uwanja wa ndege wa mji mkuu wa Yemen umeshambuliwa mara nane na ndigi za majeshi ya uvamizi ya Saudi Arabia pamoja na washirika wake nchini humo.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky