Wanajeshi 5 wa Saudi Arabia waangamia katika mipaka wa Yemen

Wanajeshi 5 wa Saudi Arabia waangamia katika mipaka wa Yemen

Serikali ya Saudi Arabia imetangaza kuangamia kwa wanajeshi wake watano katika mipaka ya Yemen na nchi hiyo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: shirika la habari rasmi la Saudi Arabia limetanga kuangamia kwa wanajeshi wake watano katika maeneo ya mipaka nchi hiyo na Yemen sehemu ya Jizan, ambapo wameuwawa baada ya mapigano makali na majeshi ya Yemn.
Kwa upande mwengine serikali ya Saudi Arabia siku ya Ijumaa imetangaza kuuwawa kwa wanajeshi wake wa usalama wawili katika mipaka ya Yemen.
Saudi Arabia iliivamia kijeshi Yemen ikishirikiana na nchi kadhaa za kiarabu na kuizingira nchi hiyo, katika anga na kila pande, ikidai kuwa hayo yote ni kwaajili ya kumrejesha Abdirabih Mansuri Hadiy ambaye ni Rais aliyekuwa amejiengua katika kuitawala Yemen.
Ambapo uvamizi huo mpaka sasa hujaleta tija yeyote iliokusudiwa na serikali ya Riyadh na washirika wake, ambapo badala yake ikawa ni sababu ya kuharibu maiundombinu ya nchi hiyo pia kusababisha mauaji makubwa ya watu wasikuwa na hatia nchini humo.   
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky