Wanajeshi kadhaa wa Saudi Arabia wafa na wengine lkujeruhiwa nchini Yemen

Wanajeshi kadhaa wa Saudi Arabia wafa na wengine lkujeruhiwa nchini Yemen

Mapigano makali yaliotokea kati ya wanajeshi wa Yemen na majeshi vamizi ya Saudi Arabia katika sehemu ya (Dhi Naim) na (Al-zahir) nchini Yemen na kusababisha vifo vya wanajeshi kadhaa wa Saudi Arabia

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: majeshi ya Yemen wamekabiliana na shambulio la majeshi vamizi ya Saudi Arabia katika sehemu ya (dhi Naim) iliopo katika mkoa wa Al-baidha, jambo ambalo limepelekea kufa watu kadhaa na wengine wengi kujiruhiwa nchini Yemen.

Aidha mizinga ya wanajeshi wa Yemen yalisambaratisha mbinu za majeshi vamizi ya Saudi Arabia katika sehemu ya Al-zahir iliopo katika mkoa wa Al-baidha nakujeruhi watu kadhaa katika majeshi ya Saudi Arabia.

Kwa mujibu wa ripoti iliotufikia, inasemekana kwamba serikali ya Saudi Arabia ikishirikiana na baadhi ya nchi kadhaa za kiarabu zilianza mashambulio yake toka miaka iliopita dhidi ya taifa la Yemen na kuizingira nchi hiyo kwa kila pande, katika anga baharini na nchi kavu kwa lengo kushinikiza kurudi katika utawala kwa Rais aliojiuzulu (Abdurabih Mansur Hadi).

Uvamizi huo mpaka sasa haujafika katika lengo lake, huku likiacha mauaji makubwa ya wananchi wasiokuwa na hatia na wengine wengi kujeruhiwa nchini humo nakuwafanya baadhi ya wanachi kuwa wakimbizi katika sehemu mbalimbali.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky