Wanajeshi watatu wa Ukraine wauawa

 Wanajeshi watatu wa Ukraine wauawa

Wanajeshi watatu wa Ukraine wameuawa na wengine 10 kujeruhiwa katika mapigano na waasi

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Wanajeshi watatu wa Ukraine wameuawa na wengine 10 kujeruhiwa katika mapigano na waasi wanaotaka kujitenga na Ukraine na kujiunga na Urusi. Hayo ni kwa mujibu wa jeshi la Ukraine katika taarifa yake ya leo. Mapigano makali yameripotiwa katika miji ya Avdiivka upande wa kaskazini na Marinka upande wa magharibi ya mji wa Donetsk ambao ni ngome ya waasi. Pande zote mbili zimelaumiana kwa machafuko hayo.Watu kadhaa wameuawa katika wiki za hivi karibuni kufuatia ongezeko la mapigano wakati Ukraine ikichukua urais wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa mwezi mmoja. Mawaziri wa mambo ya nje wa Ukraine na Urusi wanatarajiwa kukutana na wenzao wa Ujerumani na Ufaransa hapo kesho kwa mazungumzo kandoni mwa mkutano wa kimataifa kuhusu usalama mjini Munich, Ujerumani.

Mwisho wa habari/ 291

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky