Wanajeshi wawili wa Uturuki wapoteza maisha baada ya bomu kuripuka

Wanajeshi wawili wa Uturuki wapoteza maisha baada ya bomu kuripuka

Wanajeshi wawili wa jeshi la Uturuki wamepoteza maisha kufuatia kuripuka bomu liliokuwa limetengezwa kienyeji kusini mwa mashariki ya taifa hilo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: habari ya kupoteza maisha kwa wanajeshi wa Serikai ya Uturuki zimesambazwa katika vyombo vya habari mbalimbali nchini humo.
Wanajeshi hao wawili wamepoteza maisha siku ya Jumamosi kufuatia kuripuka kwa bomu liliotengezwa kienyeji kusini mwa mashariki mwa taifa hilo.
Mripuko huo ulitokea kipindi ambacho gari liliokuwa na wanajeshi wa jeshi la Uturuki wakipita katika sehemu hiyo iliopo katika mkoa wa  Batiman bchini humo.
Serikali ya Uturuki limewataja wahusika wa tukio hilo la kigaidi kuwa ni kikundi cha kigaidi cha PKK, kikundi hicho kilichokuwa na fikra za kujitenga na Uturuki kimefahamika kuwa ni cha kigaidi katika nchini mbalimbali duniani.
Maeneo ya kusini mwa mashariki mwa Uturuki kila siku kumekuwa kukitokea mashambulio baina ya kikundi hicho na majeshi ya ulinzi na usalama ya serikali ya Uturuki, ambapo mpaka sasa yamesababisha kupoteza maisha idadi kubwa ya wananchi na wanajeshi nchini humo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky