Wananchi 300 wa Azerbaijan wapoteza maisha nchini Iraq na Syria

Wananchi 300 wa Azerbaijan wapoteza maisha nchini Iraq na Syria

Serikali ya Azerbaijan leo imetangaza kupoteza maisha kwa wananchi wake 300 nchini Syria na Iraq

Shirika la habari AhlulaBayt (a.s) ABNA: serikali ya Azerbaijan leo imetangaza kupoteza maisha kwa wananchi wake 300 nchini Syria na Iraq.
Hayo yamesemwa na naibu kiongozi wa kamati masuala ya dini nchini Azerbaijan kuwa watu 92 miongoni mwa wananchi wa Azerbaijan ambao walikuwa pamoja na kikundi cha kigaidi cha Daesh wamekamatwa na kufikishwa mahakamani kwaajili ya kuhukumiwa katika mahakama ya nchi hiyo, huku watu 260 wa taifa hilo wanyanganywa utaifa wao.
Aidha ameongeza kusema kuwa: watu 300 miongoni mwa wananchi wa nchi hiyo wakiwemu wanawake na watoto wamepoteza maisha nchini Syria na Iraq baada yakujiunga na vikundi vya kigaidi katika nchi hizo.
Inasemekana kuwa magaidi wa Daesh ambao wanatoka katika mataifa mbalimbali walijiunga na kikundi cha kigaidi cha Daeh, walifanya mauaji na jinai kubwa za kigaidi nchini Iraq na Syria na kufanikiwa kuteka baadhi ya maeneo ya nchi hizo, ama baada ya kiongozi wa Dini nchini Iraq (Ayatullah Sistaniy) kutoa fatuwa ya kukabiliana na magaidi hao, kutokana na juhudi za majeshi ya Iraq na Syria na ushirikiano wao katika kukabiliana na magaidi hao, wameweza kuzikomboa sehemu ambazo zilitekwa na magaidi katika nchi hizo na kupelekea idadi kubwa ya magaidi wa Daesh kupoteza maisha.   
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky