Wanasiasa Mashuhuri wamkosoa Trump kuhusu kuzia waislam kungia Marekani

Wanasiasa Mashuhuri wamkosoa Trump kuhusu kuzia waislam kungia  Marekani

Wataalam zaidi ya 130 wa siasa ya nje wa Marekani wanapinga amri mpya ya rais Donald Trump inayowazuia watu kutoka mataifa sita ya kiislam kuingia nchini humo. Kwa madai ya ugaidi huku akiiacha Saudia arabia ambayo ndo mdhamini mkuu wa makundi ya kigaidi likiweko kundi la Al-qaeda na Daesh.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Wataalam zaidi ya 130 wa siasa ya nje wa Marekani wanapinga amri mpya ya rais Donald Trump inayowazuia watu kutoka mataifa sita ya kiislam kuingia nchini humo. Kwa madai ya ugaidi huku akiiacha Saudia arabia ambayo ndo mdhamini mkuu wa makundi ya kigaidi likiweko kundi la Al-qaeda na Daesh.

Wataalam hao wanaitaja amri hiyo kuwa ni ya "hatari kwa usalama wa taifa." Katika waraka walioitumia serikali mjini Washington, wataalam hao wanahoji kwamba uamuzi wa rais Trump kuwapiga marufuku waislam kuingia Marekani, unaikuza propaganda isiyokuwa na msingi kwamba Marekani inapigana "vita dhidi ya dini ya kiislam". Miongoni mwa waasisi wa waraka huo ni pamoja na waziri wa zamani wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Madeleine Albright, mshauri wa zamani wa masuala ya usalama wa taifa Susan Rice, waziri wa zamani wa usalama wa taifa Janet Napolitano na kiongozi wa zamani wa kituo cha kinga dhidi ya ugaidi Matthew Olsen. Balozi wa zamani wa Marekani katika jumuia ya kujihami ya NATO Nicholas Burns na msimamizi wa zamani wa rais wa zamani George W. Bush katika mapambano dhidi ya ugaidi Richard Clarke ni miongoni pia mwa waliotia saini waraka huo.

Mwisho wa habari / 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky