Wanazuoni wa Bahrain watoa wito kwa wananchi kufanya maandamano ya himaya ya Ayatullah Isa Qasim

Wanazuoni wa Bahrain watoa wito kwa wananchi kufanya maandamano ya himaya ya Ayatullah Isa Qasim

Wanazuoni wa Bahrain wametoa wito kwa wananchi wa nchi hiyo kufanya maandamano makubwa kuanzia tarehe 9 mpaka 14 ndani ya mwezi Machi kwaajili ya kumuhami Ayatullah Ahmad Isa Qasim humo

Shirika la habarai AhlilBayt (a.s) ABNA: wanazuoni wa Bahrain wametoa kauli ya kuwataka wananchi kumuhami Ayatullah Sheikh Isa, kwa kufanya maandamano makubwa kwa muda wa siku tano nchini humo, ambapo itaanza tarehe 9 mpaka tarehe 14 mwezi huu.
Matini ya kauli hiyo ni kama ifuatavyo:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema mwenye kurehemu
“ قُلْ إِنَّمَا أَعِظُكُمْ بِوَاحِدَةٍ أَنْ تَقُومُوا لِلَّهِ مَثْنَى وَفُرَادَى “
Sema kwa hakika nawawaidhini kwa (Mungu) mmoja, kwamba musimame kwaajili ya mwenyezi Mungu mukiwa wawili au pekee
Haya ni maneno ya mwenyezi Mungu kwamba huwaataka kusimama kidete kwaajili ya Mwenyezi Mungu, kwa maana aya hii ni ufunguo wa mapinduzi ambayo ameisema mwenyezi Mungu kupitia manabii wake na watu wema katika nyimati zote.
Kwani haiwezekani kufanya islahili na kutengeneza nchi na watu wake isipokuwa kwa, kusimama kidete kwaajili ya kutetea haki kwaajili ya mwenyezi Mungu na kufikia hatua ya mtu kutoa maisha yake kishujaa kwaajili yake mola muumba.
Hivyo basi witu wetu kwa wote wanaosimamia haki na kutafuta uadilifu na utukufu wa dini na nchi yake, huu ndio wakati wenu enye wana wa Bahrain, hii ni fursa muhimu ya kufikia matashi yenu, hivyo munapaswa kusimama kwaajili ya Mungu ambapo mtarehemewa na Mwenyezi Mungu.
Enye taifa lilio na Imani na kumyegemea mwenyezi Mungu mtukufu, tunawataka tufanye maandamano makubwa kuanzia tarehe 9 mpaka 14 ya mwezi huu, ambayo ndio siku ya kuhukumiwa shahsia kubwa ya kiroho na imani Ayatullah sheikh Ahmad Isa Qasim, na kuifanya siku hiyo kuwa ni siku ya kihistoria nchini kwa kushiriki kwenu katika maandamano haya makubwa huku tukiwa na kauli mbiu hizi “haturudi majumbani mwetu”, “tutamuhami hata kwa kutoa roho zetu” ambapo kwa kufanya hivyo tutakuwa wenye kuinuru dini na Imani na taifa letu kutokana na dhulma na ufasiki.
“na yeyute atakayetoka nyumbani kwake kwaajili ya mwnyezi Mungu na Mtume wake, hatimaye kumpata umauti, basi bilashaka mtu huyo malipo yake yako kwa mwenyezi Mungu”.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky