Watalii wawili wa Ujerumani wauliwa nchini Misri

 Watalii wawili wa Ujerumani wauliwa nchini Misri

Kijana mmoja wa Misri ameuwa watu watalii wawili wanao sadikiwa kuwa ni wananchi wa Ujerumani, ambapo tukio hilo limetokea katika moja ya Hotel ziliopo nchini Misri

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kijana mmoja asiefahamika nchini Misri aliwashambulia watalii 6 wakike ambao ni raia wa Ujerumani katika moja ya Hotel za kitalii za Hurghada nchini humo, hatimaye kuuwa watu wawili kati yao na wengine kadhaa kuwajeruhi nchini humo.
Shirika la habari la Reuters likinukuu kutoka kwa kamanda Muhammad Al-hamzawi, msimamizi wa masuala ya usalama sehemu hiyo na kusema kuwa: kijana huyo alitumia kisu katika kuuwa watalii hao wawili wa kijerumani waliokuwa katika Hotel moja ya kitalii nchini Misri.
Vyanzo vya usalama vya sehemu hiyo kabla ya hapo vilitangaza kuwa wanawake wawili ni wananchi wa Ukrainem, kadhalika kiongozi wa vyombo vya usalama wa sehemu hiyo ametangaza kuwepo wanawake wawili ambao ni wananchi wa Czechia katika majeruhi wa tukio hilo.
Walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa: kijana mmoja asiofahamika aliwashambulia watu kutoka mataifa ya kigeni nchini Misri katika sehemu moja ya kitalii na baadae kukimbia kwa kuruka ukuta na kwenda katika Hotel nyingine ya kitalii iliopo karibu na sehemu hiyo na huko pia kuwajeruhi watu wengine.
Aidha wameongeza kusema kuwa majeshi ya ulinzi ya nchi hiyo walifanikiwa kumkamata mtu huyo na kumkabidhi katika idara husika ya usalama kwaajili ya uchunguzi ili lifahamike kusudio lake la kufanya tukio hilo. Huku majeruhi hao wakichukuliwa na kukimbizwa hospitalini kwaajili ya kupata matibabu.

mwisho/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky