Watoto 180 wafa kwa ugonjwa wa kipindupindu nchini Yemen

Watoto 180 wafa kwa ugonjwa wa kipindupindu nchini Yemen

Wizara ya afya nchini Yemen imetangaza kuhitaji vitanda elfu nane vya Hospitali ili kuweza kukabiliana na kuene kwa ugonjwa huo nchini humo

Shirika la habari AhlulaBayt (a.s) ABNA: chama cha msalaba mwekundu duniani kimetangaza kuwa watu 180 wamekufa nchini Yemen kufuatia ugunjwa wa kuambukiza wa kipindupindu.
Aidha chama hicho kimebainisha kuwa, watu waliokufa kufuatia ugonjwa huo ni watoto wadogo, huku wakisisitiza kuwa hali ya kiafya ya nchi hiyo inazidi kuwa mbaya kutokana na kuenea vikali kwa ugunjwa huo.
Wizara ya afya nchini humo imebainisha kuwa: ili kuweza kukabiliana na kuenea kwa ugunjwa huo, nchi hiyo inahitaji vitanda elfu nane vya hospitali vitakavyo wezesha kukabiliana na janga hilo.
“Nasir Al-arjiliy” naibu waziri wa afya na msimamizi wa masuala ya madawa nchini Yemen alipokuwa katika mahuojiano na Televishen ya Almayadin amesema kuwa: wizara ya afya na tiba nchini humo haina uwezo wa kukabiliana na kasi ya kuenea kwa ugunjwa huo kutokana na kuendelea kwa vita na kufungwa kwa Bank kuu ya nchi hiyo.
Aidha ameitaka jumua za kimataifa kuisaidia Yemen katika kubiliana na kuene kwa ugujwa huo katika taifa hilo, huku wezara ya hiyo ikiashiria kuwa waliopatwa na ugunjwa huo nchini humo ni watu elfu 12.
Msimamizi wa masuala ya kibinadamu katika ofisi ya umoja wa Mataifa nchini Yemen imesisitiza kuwa kutokana na kufungwa kwa asilimia 50 ya vituo vya afya katika maeneo mbalimbali nchini humo, kutapelekea kushadidi kwa ugunjwa huo nchini humo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky