Watu 15 wafariki na 23 kujeruhiwa katika mripuko uliotokea katika shule nchini Iraq

Watu 15 wafariki na 23 kujeruhiwa katika mripuko uliotokea katika shule nchini Iraq

Shule moja aliokuwa imetegwa bomu katika kijiji kimoja vha Majarin ambapo kuna umbali wa kilometa 20 kufika magharibi mwa Musol nchini Iraq yaripuka na kusababisha vifo vya watu 15 na wengine 23 kujeruhiwa kufuatia mripuko huo.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: katika mripuko huo uliotokea katika shule iliokuwa imetegwa Bomu katika kijiji cha Majarin, kilometa 20 kufika magharibi mwa Musol, umesababisha vifo vya wanajeshi 12 wa jeshi la kujitolea nchini humo.
Hayo yamesemwa na Jabaru Al-maamuriy, mmoja katika makamanda wa majeshi ya kujitolea katika kukabiliana na kikundi cha kigaidi cha Daesh amesema kuwa: mripuko huo ulitokea ndani mwa shule hiyo na kusababisha vifo vya watu 15 ambapo 12 kati yao ni wanajeshi wa kujitolea, huku watu 23 miongoni mwa wanajeshi hao kujeruhiwa.
Magaidi wa kikundi cha kigaidi cha Daesh walitega bomu hilo katika shule  hiyo kabla hawaja ondoshwa katika mji waMusol nchini Iraq.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky