Watu 40 wauwawa kutokana na milipuko ya mabomu Syria

Watu 40 wauwawa kutokana na milipuko ya mabomu Syria

Watu wapatao 40 wameuwawa kutokana milipuko miwili ya mabomu katika mji mkuu wa Syria, Damascus.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Watu wapatao 40 wameuwawa kutokana milipuko miwili ya mabomu katika mji mkuu wa Syria, Damascus.

Shirika la habari la taifa nchini Syria SANA limeripoti kuwa milipuko hiyo imetokea karibu na eneo lenye makaburi la Bab al-Saghir mojawapo ya maeneo ya kale ambapo viongozi mashuhuri wa kidini wamezikwa. Taarifa hizo zinaeleza kwamba mbali na watu kuuwawa eneo hilo la makaburi limeharibiwa vibaya pia. Wakati huo huo rais wa Syria Bashar al Assad amesema lengo kuu la jeshi lake ni kuukomboa mji wa Raqqa ambao ni ngome ya kundi la kigaidi la Daesh linalojiita Dola la Kiislamu. Rais Assad aliyasema hayo alipofanyiwa mahojiano na televisheni ya China inayoendesha kazi zake katika mji wa Phoenix nchini Marekani. Assad alisema serikali yake inapanga kuendeleza operesheni sambamba na ya mji wa Raqqa dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh katika mji wa Dier el Zour ambao pia ni ngome ya magaidi hao.

Wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh wamedhoofika vibaya na kupeteza maeneo mengi yalikuwa katika himaya yao nchini Syria, ambapo majeshi ya Iran na Urusi yanasaidia majeshi ya Syria katika kupambana na magaidi hao hatari wanaodhaminiwa na muungano wa mataifa ya kiarabu na magharibi.

Mwisho wa habari/ 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky