Watu 400 waliokimbia makazi yao warejea pembezoni mwa mji wa Aleppo nchini Syria

Watu 400 waliokimbia makazi yao warejea pembezoni mwa mji wa Aleppo nchini Syria

Wizara ya ulinzi na Uslama ya Urusi imetangaza kwamba toka muda ambao kikundi cha kigaidi cha Daesh kushindwa nchini Syria, zaidi ya wananchi 400 waliokuwa wamekimbia makazi yao, wameonekana kurudi katika makazi yao ya awali pembeni mwa mji wa Aleppo nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA:  wizara ya ulinzi na Uslama ya Urusi imetangaza kwamba toka muda ambao kikundi cha kigaidi cha Daesh kushindwa nchini Syria, zaidi ya wananchi 400 waliokuwa wamekimbia makazi yao, wameonekana kurudi katika makazi yao ya awali pembeni mwa mji wa Aleppo nchini humo.
Aidha imeelezwa kwamba, kurudi kwa watu hao waliokuwa wamekimbia sehemu hizo, kumeanza baada ya majeshi ya Syria kufanikiwa kuyamiliki maeneo hayo na kuwa chini yao.
Wizara ya ulinzi ya Urusi imeashiria kuwa kurudi kwa wananchi hao katika nyumba zao katika maeneo mbalimbali ya mji wa Aleppo, sehemu ambazo hapo awali yalikuwa chini ya vikosi vya Wakurdi, ambapo hivi sasa kumeweza kupatikana muafaka baina ya vikosi hivyo na majeshi ya Syria, kupitia chama cha suluhisho cha Urusi.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky