Watu 53 wauwawa na kujeruhiwa kwa tukio la kigaidi nchini Ujerumani

Watu 53 wauwawa na kujeruhiwa kwa tukio la kigaidi nchini Ujerumani

Vyombo vya habari nchini Ujerumani vimetangaza kutokea shambulio la kigaidi magaharibi mwa Ujerumani ambapo kufuataia shambulio hilo watu kadhaa wameuwawa na wengine kujeruhiwa.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: vyombo vya habari vya Ujerumani vimetangaza kuwwa gari moja liliokuwa barabarani katika barabara za mji wa Munster nchini humo limewakanyaga watu kadhaa na kusababisha kupteza maisha na kujeruhiwa, ambapo mpaka sababu ya kutokea kwa ajali hiyo bado haijafahamika.
Jeshi la Polisi nchini Ujerumani likitoa kauli kuhusu tukio hilo wamesema: tukio hilo ni la kigaidi ambapo baada ya kufanywa kwa tukio hilo, deleva aliyekuwa anaendesha gari hilo alijiuwa.
Aidha vyombo vya habari nchini Ujerumani kufuatia ripoti ya awali iliotolewa ni kwamba watu 50 wameuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Majeshi ya Ujerumani yaliwahi kufika katika tukio hilo, hiko jeshi la polisi nchini humo limetangaza kuwa dereva wa gari hilo baada ya kufanya tukio hilo alijipiga risasi hatimaye kupoteza maisha papo hapo.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky