Wananchi 64 wauwawa kufuatia shambulio la masnaipa wa Daesh katika mji wa Musol

Wananchi 64 wauwawa kufuatia shambulio la masnaipa wa Daesh katika mji wa Musol

Watu 64 ambao ni wakazi wa mji wa Musol wauwawa kikatili wakiwemo wanawake na watoto ambao walikuwa wakikimbia kutoka katika mji huo na kutafuta mahala palipokuwa na amani kwaajili ya kuokoa roho zao, ambapo masnaipa wa kikundi cha Daesh kuwawinda kwa risasi

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: jinai zingine za kikundi cha kigaidi cha Daesh zadhihiri nchini Iraq, ambapo watu wasiopungua 64 ambao ni miongoni mwa wakazi wa mji wa Musol wauliwa kinyama na Masnaipa (Snipers) wa kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini humo.
Idadi kadhaa ya wananchi wasiokuwa wanajeshi nchini Musol wameuwawa siku ya Alhamisi ya tarehe 11 mwezi huu, ambapo wananchi hao walikuwa wanakusudia kukimbiakatika maeneo yanayokaliwa na vikundi vya kigaidi vya Daesh wakivuka katika mto wa Tigris kwenda katika sehemu iliokuwa na amani, ama magaidi hao hawakuwaacha wananchi wasiojiweza hatimaye kuwawinda kwa silaha nzito na kupoteza maisha.
Wananchi waliookoka na mashambulio ya magaidi hao wamesema kuwa idadi ya waliopoteza maisha ni zaidi ya 64, ama baada ya kutokea tukio hilo maiti zilionekana na katika mtu huo ni watu 64, huku ikisadikiwa kuwa watu walipigwa risasi hizo na kuangukia katika mto huo ni zaidi ya famialia arubaini.
Kamanda wa jeshi la Polisi la Iraq katika mji wa Musol amesema: mpaka sasa wameokota maiti 64 katika mto wa Tigris, huku miili hiyo ikiwa na athari ya risasi ziliopigwa na kikundi cha kigaidi cha Daesh.
Aidha aliendelea kusema kuwa: tunaamini kuwa idadi ya waliopoteza maisha ni zaidi ya hao waliopatakana na hivi sasa tunaendelea kufanya uchunguzi kuhusu miili mingine.
Toka muda yalioanza mashambulizi kuukomboa mji wa Musol kutoka mikononi mwa kikundi hicho cha kigaidi, mamia ya wakazi wa mji huo wamefanikiwa kutoka kufuatia msaada wa majeshi ya nchi hiyo kutoka maeneo yanayo kaliwa na kikundi hicho cha kigaidi nchini Iraq.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky