Watu walio na silaha washambulia jeshi la Polisi mjini Cairo

Watu walio na silaha washambulia jeshi la Polisi mjini Cairo

Watu wawili waliokuwa na silaha ambao walikuwa ndani ya gari wameshambulia jeshi la Polisi kwa risasi nchini Misri katika mji mkuu wa nchi hiyo mjini Cairo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: watu wasiofahamika mjini Cairo, wameshambulia jeshi la Polisi na kusababisha vifo vya Polisi watatu na wengine watano kujeruhiwa
Wizara ya mambo ya ndani ya Misri imetangaza hayo katika kauli iliotolewa na wizara hiyo na kusema kuwa: shambulio hilo limefanyika nyakati za saa sita ya usiku, ambapo watu walikuwa ndani ya gari walifyatua risasi kwa askari wa jeshi la Polisi la nchi hiyo, ambapo pia majeshi ya Polisi nayo yalijibu mashambulizi hayo kwa kuwarushia risasi.
Kwa mujibu wa kauli hii ya wizara ya mambo ya ndani, mashambulio hayo yametokea katika moja ya Madinat Nasr mashariki mwa mji wa Cairo na kupelekea kuuwawa polisi wawilili papohapo. Mpaka sasa hakuna kikundi chochote cha kigaidi kilichotangaza kuhusika na shambulio hilo la kigaidi.
Vikundi vya kigaidi nchini humo vilianza mashambulizi yake dhidi ya majeshi ya nchi hiyo toka miaka mine iliopita, katika maeneo ya kaskazini mwa jangwa la Sinai, ambapo mashambulio hayo yalisambaa kutoka kaskazini mwa Sinai kwenda mji mkuu wa nchi hiyo hata kufikia katika miji ya Delta iliopo nchini Misri.  
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky