Watu watatu wajeruhiwa kufuatia shambulio la kombora la majeshi ya Yemen kusini mwa Saudia

Watu watatu wajeruhiwa kufuatia shambulio la kombora la majeshi ya Yemen kusini mwa Saudia

Majeshi ya Yemen siku ya Ijumaa yametangaza kufanya shambulio lake la makombora kadhaa yaliolenga sehemu ya (AL-aridha) katika mkoa wa Jizani kusini mwa Saudi Arabia

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: taarifa ya kufanywa shambulio la makombora yaliofanywa na majeshi ya Yemen nchini Saudi Arabia.

Majeshi ya Yemen siku ya Ijumaa yamefanya mashambulio kadhaa katika sehemu ya Al-Aridha katika mkoa wa Jizani kusini mwa Saudi Arabia.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Saudi Arabia kwama mashambulio hayo yamesababisha kujiruhiwa watu watatu nchini humo.

Aidha vyombo vya habari vya Yemen vimetangaza kuwa: mashambulio ya makombora hayo yalikuwa yamelenga kambi za wanajeshi katika mkoa wa Jizan nchini Saudi Arabia.

Kwa mujibu wa habari hii, kadhalika sehemu ya jangwa la Almisyal katika mkoa wa Asir uliopo kusini mwa Saudi Arabia pia ulishambuliwa kwa makombora hayo ya wanajeshi wa Yemen.

Kwa upande mwingine ndege za kijeshi za Saudi Arabia siku ya Ijumaa zimeshambulia mara kadhaa katika mji mkuu wa Yemen, huku ikielezwa kuwa mashambulio hayo yamepelekea kuuwawa wananchi kadhaa na wengine wengi kujeruhiwa.

Majeshi ya Saudi Arabia toka miaka miwili iliopita yalianza mashambulio makubwa nchini Yemen, kwa lengo la kuyamiliki maeneo mbalimbali nchini Yemen, ambapo majeshi ya Yemen yalilazimika kukabiliana na mashambulio hayo, hatimaye majeshi ya Saudi Arabia mpaka sasa kushindwa kufikia malengo yake nchini humo.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky