Watu zaidi ya 60 wauwawa na kujeruhiwa nchini Yemen kwa shambulio la majeshi ya Saudia+ picha

 Watu zaidi ya 60 wauwawa na kujeruhiwa nchini Yemen kwa shambulio la majeshi ya Saudia+ picha

Zaidi ya watu 60 wamepoteza maisha na kujeruhiwa nchini Yemen ikiwemu watoto na akina mama kufuatia mashambulio ya anga yaliofanywa na majeshi ya serikali ya Saudi Arabia

Shirika la habari AhlulaBayt (a.s) ABNA: ndege za kivita za Saudi Arabia zafanya jinai zingine katika sehemu ya Haran katika mkoa wa Hajjah ambapo kufanya mashambulizi hayo watu zaidi ya 60 wamepoteza maisha na kujeruhiwa nchini humo.
Vyanzo vya kidaktari nchini Yemen viimetangaza kupoteza maisha na kujeruhiwa kwa watu zaidi ya 60 katika mashambulio hayo ya kinyama huku wakisisitiza kuwa miongoni mwa waliopoteza maisha watu 10 ni waokoaje wa majeruhi ambao ndege za Saudi Arabia hazikuwacha kuwashambulia hata waokoaji hao.
Msemaji wa wizara ya Afya nchini humo mashamhulizi yalishadidi siku iliopita kwamba ndege za kivita za Saudi Arabia zilishambulia sehemu ya Haran katika mkoa wa Hajjah, ambapo mashamulio hayo inaonyesha wazi kuvunja sheria za haki za binadamu na sheria za kimataifa kidini kibinadamu hata kidini.
Aidha ameendelea kusema kuwa kushambulia wananchi wasiokuwa na hatia ikiwemo watoto, wanawake, vijana na wazee kwa masaa kadhaa kwa kushambulia makazi ya wananchi hao ni suala lisilokubalika kitabia na kibinadamu.
Mwisho amewataka walimwengu kuto yafumbia macho mauaji hayo na kukaa kimya badala yake kupaza saudi ya kuilazimisha serikali ya Saudi Arabia kuacha kufanya vitendo hivyo vya kinyama.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Arba'een
Mourining of Imam Hossein
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky