Watu zaidi ya laki mbili wapatwa na ugonjwa wa kipindupindu nchini Yemen

Watu zaidi ya laki mbili wapatwa na ugonjwa wa kipindupindu nchini Yemen

Jumuia ya umoja wa mataifa siku ya Alhamisi sawa na tarehe 6 mwezi huu imetangaza kuwa: watu waliopatwa na ugonjwa wa kipindupindu wafikiwa laki mbili na thamanini na nne elfu nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: ugonjwa wa kipindupindu bado unazidi kusambaa nchini Yemen, ambapo jumuia ya umoja wa kimataifa nchini humo umetangaza:idadi ya watu waliopata ugonjwa huo wafikia laki mbili na thamanini na nne elfu.
Aidha ameendelea kubainisha kuwa miongoni mwa idadi hiyo iliashiria wato 1657 wamefariki dunia kwa ugunjwa huo, huku akiashiriwa kuwa asilimia 25 ya waliopatwa na ugunjwa huo ni watu waliokuwa na umri kuanzia miaka 15 kushuka na asilimia 30 ya watu wanaopatwa na ugonjwa huo ni watu wazima waliokuwa na umri wa miaka 60.
Jumuia ya umoja wa mataifa ametoa tahadhari kunako kuendelea kuenea kwa ugonjwa huo nchini Yemen na kuongezeka kwa idadi ya waathirika nchini humo.
Asilimia 45 ya vituo vya afya nchini Yemen vimefungwa na kuto fanya kazi nchini humo kufuata vita ya miaka miwili inayoendelea nchini humo, alkadhalika vituo viliobaki pia havifanyi kazi ipasavyo kitu ambacho kinasababisha kudhoofika harakati za kukabiliana na ugonjwa huo hatari ambao mpaka sasa umesababisha kupoteza maisha ya wananchi wengi wa nchi hiyo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky