Wawili waliokuwa na silaha wauwawa na Polisi nchini Misri

 Wawili waliokuwa na silaha wauwawa na Polisi nchini Misri

Jeshi la polisi nchini Misri lauwa watu wawili waliokuwa na silaha katika mapigano yaliotokea katika mkoa wa “Al-Gharbia” nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: habari za kuuwawa kwa watu wawili waliokuwa na silaha nchini Misri zatangazwa, ambapo jeshi la Polisi nchini humo limetangaza kuwaua watu hao katika mapigano yaliotokea katika mkoa wa Al-Gharbia.
 kwa mujibu wa ripoti ya wizara ya mambo ya ndani nchini humo, watu hao wanafungamano la karibu na kikkundi cha majeshi ya Ikhwanul Muslaimina nchini nchini Misri.
Watu hao wawili waliokuwa na silaha walianza kuwarushia risasi askari waliokuwa wanakaribia katika maficho yao, ndipo jeshi la Polisi la nchi hiyo likaanza mapambano dhidi ya watu hao, ampapo baada ya kuuwawa kwa watu hao walifanya uchunguzi katika maficho yao na kuona silaha mbili nzito na baadhi ya vifaa vingine.
Kwa mujibu wa ripoti ya wizara ya mambo ya ndani ya Misri imesema kuwa: watu hao waliokuwa na silaha kazi yao ilikuwa ni kutengeza mabomu na kuyasafirisha kwenda kwa vikundi viliokuwa na silaha viliokuwa na fungamano na kikundi cha Ikhwanul Muslimina nchini humo.
Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo amesema kuwa vikundi viweli viliokuwa na silaha “Hasmi” na “liwau Thawrah” ambavyo vinafungamano na kikundi cha Ikhwanul Muslimina, ambapo harakati za vikundi hivyo hairuhusiwi nchini humo.
Kikundi kilichokuwa na silaha cha (Hasm) wiki iliopita kilitangaza kuhusika na mauaji ya askari Polisi watatu katika shambulio waliofanya katika mji mkuu wa Cairo, hivi karibuni miji mbalimbali ya Misri imeshudia mashambulio mbalimbali kutoka vikundi viliokuwa na silaha nchini humo, ambapo yamesababisha kuifanya nchi hiyo kupoteza amani yake iliokuwepo hapo kabla.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky