Waziri mkuu wa Iraq: mji wa Musol umekombolewa kikamilifu

Waziri mkuu wa Iraq: mji wa Musol umekombolewa kikamilifu

Waziri mkuu wa Iraq amewasili katika mji wa Musol na kutangaza ushindi wa nchi hiyo dhidi ya kikundi cha kigaidi cha Daesh nchni humo

Shirika la habari AhlulByt (a.s) ABNA: kamanda mkuu wa Iraq ametangza kuwa: Haidar Al-abadiy ambaye ni waziri mkuu wa Iraq amewasili mjini Musol kwaajili ya kutangaza rasmi kukombolewa kwa mji huo kutoka mikononi mwa kikundi cha kigaidi cha Daesh.
Aidha amewasili mjini Musol kwaajili ya kutoa pongezi kwa wananchi wa nchi hiyo kwa ushindi mkubwa walioufikia katika mji  huo dhidi ya kikundi cha kigaidi cha Daesh, hatimaye alituma salamu za pongezi hizo kwa kufanikiwa kuukomboa mji huo.
Vita vya Musol vilianza kwa lengo la kuwatoa magaidi wa Daesh walikuwa katika sehemu hiyo, ambapo vita hiyo ilianza toka miezi 9 iliopita na siku kadhaa ziliopita majeshi ya nchi hiyo walikuwa wamesafisha sehemu hiyo kotokana na kuwepo magaidi wa Daesh na kubaki semu ya mji wa zamani ya mji huo iliopo karibu na mto wa dajla nchini humo.
Ama baada ya kufika siku ya jumamosi kukatangazwa kukombolewa kwa mji huo kwa ukamilifu kwa mji huo mpaka sehemu ya mji wa zamani wa sehemu hiyo, ambapo kwa mujibu wa maelezo ya viongozi wa serikali ya Iraq ni kwamba magaidi 30 wa kikundi cha kigaidi cha Daesh walitaka walitaka kukimbia kupitia mto wa Tigris na baada ya mapigano makali na majeshi ya Iraq magaidi hao wameuliwa wote siku ya leo, ndipo ikatangazwa kukombolewa kamili kwa mji huo.
Kikundi cha kigaidi cha Daesh kilitangaza kuumiliki mji huo uliopo kaskazini mwa Iraq toka mwaka 2014, hatimaye kikundi cha kigaidi cha Daesh kilitangaza kuwa mji huo ndio makao makuu ya utawala wa kigaidi wa kikundi hicho.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky