Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anakutana na rais wa Urusi Vladimir Putin mjini Moscow leo, ambapo wanatarajiwa kuzung

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anakutana  na rais wa Urusi Vladimir Putin mjini Moscow leo, ambapo wanatarajiwa kuzung

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anakutana na rais wa Urusi Vladimir Putin mjini Moscow leo, ambapo wanatarajiwa kuzungumzia ongezeko la nguvu na ushawishi wa Waislamu wa dhehebu la shia Mashariki ya Kati ambao ni maadui wakubwa wa Israel.

Shirika la habari la ABNA linaripoti  kuwa: Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anakutana  na rais wa Urusi Vladimir Putin mjini Moscow leo, ambapo wanatarajiwa kuzungumzia ongezeko la nguvu na ushawishi wa Waislamu wa dhehebu la shia Mashariki ya Kati ambao ni maadui wakubwa wa Israel.

Israel na Marekani kwa  kushirikiana Uturuki na mataifa ya kiarabu yakiongozwa na Saudia Arabia wamekuwa wakidhamini makundi ya kigaidi nchini Syria kwa lengo la kuiangusha serikali ya Syria ambayo ilikuwa inalisaidia kundi la wanaharakati wa Hibullah ambao waliishinda Israel katika vita vya mwaka 2006, jambo lililopelekea kuundwa makundi haya ya kigaidi ili kuangusha serikali ya Syria na kuidhoofisha Iran na makundi ya wanamgambo yanayopingana na Israel ambayo yanadhaminiwa na Iran.

Kabla kuelekea Moscow, Netanyahu katika taarifa alisema, mazungumzo yake na Putin ni muhimu mno kwa usalama wa Israel na kwamba anapinga vikali uwepo wa Iran nchini Syria.

Kikosi wanajeshi cha Iran na wanamgambo wa kishia, Hezbollah, ambao wote ni maadui wa Israel, wote wanamuunga mkono rais wa Syria Bashar Al Assad katika mapigano dhidi ya magaidi wanaoungwa mkono na Marekani yanayoendelea nchini humo.

Urusi inamuunga mkono pakubwa Assad na kuingilia kwake vita vya Syria, kulisaidia kulibadili wimbi la vita hivyo ambavyo sasa magaidi wanaodhaminiwa na Marekani, Israel, na nchi za kiarabu wamedhoofika na kuelekea kushindwa kabisa vita hivyo.

Mbali na taarifa hiyo aliyoitoa Netanyahu, waziri mkuu huyo aliliambia bunge la Israel pia kwamba ananuia kukubaliana na Urusi kuhusiana na mzozo wa Syria katika mazungumzo hayo.  Israel imekuwa ikitumia ndege zake za kivita mara kwa mara kuwashambulia wanajeshi wa Syria ili magaidi wasonge mbele na kuchukua nchi.

Uwepo wa majeshi ya Iran nchini Syria unaashiria mwisho wa Israel

"Kuna jaribio la Iran kukita kambi kabisa nchini Syria wakiwa na majeshi ya ardhini na majini,"alisema Netanyahu, jambo linaloonekana kuwa kitisho kikubwa kwa Israel. "Kuna jaribio pia la kuweka kikwazo dhidi yetu katika eneo la Golan, nitaonyesha pingamizi kubwa kwa uwezekano huu," aliongeza Netanyahu. Golan ni eneo la milima lilipo Syria ambalo limenyakuliwa na kukaliwa kwa mabavu na majeshi ya Israel ambapo kwa sasa wanajeshi wa Iran wanaonekana kuweka kambi karibu na eneo hilo, jambo linaloinyima usingizi Israel.

Katika wiki za hivi majuzi Israel imeonesha jinsi inavyozingatia kwa umakini kitisho hichi. Gazeti la the Times nchini Israel liliripoti kwamba Januari 8, Israel ilifanya mashambulizi kadhaa katika eneo la Golan lililokuwa na wanamgambo wa kishia wa Hezbollah.

Kulingana na mshauri wa usalama wa ngazi ya juu Chagai Tzuriel, hali nchini Syria na matokeo yake ni ya umuhimu mkubwa kwa Israel. "Syria ni eneo muhimu mno, mataifa yenye nguvu kama Urusi na Marekani yako huko, na hata mataifa makubwa mashariki ya kati kama Uturuki na Iran. Isitoshe kuna makundi hasimu nchini humo, kama uongozi wa Assad, upinzani, Wakurdi na makundi ya kigaidi ," alisema Chagai.

Mayahudi wapinga adhana, wanasema adhana huleta usumbufu kwa wasio Waislamu

Wakati huo huo, bunge nchini Israel Jumatano, lilipitisha katika awamu ya kwanza miswada miwili itakayozuia misikiti kuadhini, ishara ya kuwaita Waislamu kwa sala, huku mswada mmoja ukitaka misikiti izuiwe kabisa kutumia spika kwa adhana Palestina.

Mswada huo wa pili ambao unanuia kupiga marufuku utumizi wa spika kuadhini katika miji kuanzia saa tano usiku hadi saa moja asubuhi, utafanyiwa marekebisho, huku kukiwa kumesalia vikao vitatu vya kuijadili miswada hiyo kabla haijakuwa sheria.

Miswada hiyo iliidhinishwa baada ya wabunge wa muungano tawala na wenzao wa Kiarabu kubishana vikali, hali iliyopelekea baadhi ya wabunge kuzipasua karatasi za mswada huo na kutimuliwa bungeni.

Huku miswada hiyo kimaandishi ikiwa inalenga maeneo yote ya kuabudu, Waislamu wanasema nia yake ni kutilia kikomo adhana misikitini, jambo ambalo limekuwa likifanywa tangu jadi.

Wanaounga mkono hatua hiyo ya bunge wanasema, inanuia kuzuia usumbufu kwa maelfu ya Waisraeli ambao sio Waislamu.

Rasimu ya kwanza iliyokuwa inalenga kudhibiti sauti za ving’ora vya mayahudi, ilikataliwa na bunge wakiamini kwamba adhana pekee ndio inauzi watu na si ving’ora vya mayahudi.

Israel ambayo ilichukua kwa nguvu ardhi za waislamu wa Palestina, Syria na Lebanon na kuunda taaifa liitwalo Israel kwasasa imekuwa ikiishi katika hofu kubwa baada ya majeshi ya Iran kuingia Syria, ambapo Iran inapinga vikali uwepo wa Israel katika raman ya dunia, na imeahidi kuiangamiza Israel na kuwarudishia haki zao wapalestina na wote waliodhulumiwa.

Mwisho wa habari / 291

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky