Waziri mkuu wa Uingereza: Iran haijakiuka masharti ya makubaliano ya Nyuklia

Waziri mkuu wa Uingereza: Iran haijakiuka masharti ya makubaliano ya Nyuklia

Waziri mkuu wa Uingereza alipokuwa anafanya mahojiano na Televishen ya CBS na kubainisha kuwa kutokana na anavyo amaini yeye kuwa, Iran imetekeleza ahadi yake katika kutekeleza masharti ya makubalianao ya mpango wa Nyuklia hivyo hatuna budi kuyalinda makubaliano na muafaka huo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA:   hayo yamesemwa na wazi mkuu wa Uingereza na kubainisha kuwa kutokana na anavyo amaini yeye ni kwamba, Iran imetekeleza ahadi yake katika kutekeleza masharti ya makubalianao ya mpango wa Nyuklia hivyo hatuna budi kuyalinda makubaliano na muafaka huo, kwani kufanya hivyo ndio kutazuia Iran kutengeza silaha za Nyuklia.
Aidha waziri Huyo amefafanua kuwa, sisi tunatofautiana na serikali ya Marekani katika suala hili kunako kukabiliana na Iran katika masuala mengine (yasiokuwa katika makubaliano), kwa maana kuhusu makombora ya masafa marefu yanayotengezwa na Iran ni suala liliokuwa nje ya makubaliano ambapo inabidi kufanya uchungu wa kina kunako jambo hilo.
Ama kuhusu suala la makubaliano ya mpango wa Nyuklia tuna yakini kuwa makubaliano hayo yataendelea kuwa na  nguvu yake kwani ndio njia Pekee itakayoifanya Iran isiweze kuzalisha silaha za Nyuklia.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky