Waziri wa mambo ya nje wa Iran aonana na katibu mkuu wa umoja wa Mataifa katika kikao cha Shanghai

Waziri wa mambo ya nje wa Iran aonana na katibu mkuu wa umoja wa Mataifa katika kikao cha Shanghai

Waziri wa mambo ya nje wa Iran ambaye hivi sasa yuko Kazakhstan leo ameonana na katibu mkuu wa umoja wa mataifa nchini humo.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Muhammad Javad Zarif (waziri wa mambo ya nje wa Iran) ambaye hivi sasa yuko nchini Kazakhstan, ameonana na katibu mkuu wa umoja wa mataifa na kufanya mazungumzo mbalimbali katika kikao hicho.
Katika kikao hicho katibu mkuu wa umoja wa mataifa baada ya kulaani tukio la kigaidi liliotokea mjini Teheran pia alitoa salamu za rambirambi kwa wahanga wa tukio hilo nchini humo.
Pande mbili hizo katika mazungumzo yao walizungumzia masuala ya kimataifa ya ukanda wa mashariki ya kati, hali halisi ya taifa la Syria, Iraq na Yemen.
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa amesema: njia pekee ya kutatua matatizo yaliotokea katika baadhi ya mataifa ya Ghuba ya uajemi ni kufanya mazunguzo ya kisiasa baina ya bande husika.
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa ameashiria suala la makubaliano ya nyuklia baina ya Iran na kundi la 5+1 akisema kuwa: kazi kubwa ya umoja wa mataifa ni kuhakikisha yanatekelezwa yale yote yaliokubaliwa na kuandikwa katika makubaliano hayo, huku akisistiza kuwa makubaliano ya nyuklia ya Iran ni jambo la kihistoria kutokana na umhimu wake.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky