Waziri wa mambo ya nje wa Iran aonana na waziri wa mambo ya ndani wa Pakistan

 Waziri wa mambo ya nje wa Iran aonana na waziri wa mambo ya ndani wa Pakistan

Waziri wa mambo ya nje wa Iran akiwa na jopo la baadhi ya viongo wa Iran wamewasili nchini Pakistan kwaajili ya kufuatilia tukio la kigaidi liliotokea katika mpaka wa Iran na Pakistan na kusabaisha kuuwawa kwa baadhi ya wanajeshi wa Iran, nao baada ya kuwasili wamefanya mazungumzo na waziri wa mambo ya ndani wa Pakistan mjini Islamabad

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: waziri wa mambo ya nje wa Iran baada ya kuwasili mjini Islamabad amefanya mazungumzo na waziri wa mambo ya ndani wa Pakistan
Waziri wa mambo ya nje ya Iran katika safari yake ambayo imetokea baada ya tukio la kigaidi liliotokea katika mpaka wa Iran na Pakistan, ambapo lengo la msafara huo ni kufuatilia na kufanya uchunguzi wa tukio hilo kwa undani zaidi, alkadhalika watazungumzia jinsi ya kuweka mikakati ya kuimarisha ulinzi katika sehemu hiyo na kufunga njia zinazotumika na vikundi vya kigaidi katika kufanya matukio ya kigaidi.
Muhammad javadi ZAarif (waziri wa mambo ya nje wa Iran) amewasili nchini pakistan asubuhi ya Jumatano akiwa na jopo la baadhi ya viongozi wa mambo ya kisiasa na kijeshi na usalama, ikiwa ni katika kufuatilia tukio la kigaididi liliotokea katika mpaka wa Iran na Pakistan.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky