Waziri wa mambo ya nje wa Urusi: ishara kubwa zinaashiria kuwa kiongozi wa Daesh amekufa

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi: ishara kubwa zinaashiria kuwa kiongozi wa Daesh amekufa

Waziri wa mambo ya nje ya Urusi imesema: kwa asilimia kubwa tunaweza tukathubutu kusema kuwa Al-Baghdadi mkuu wa kikundi cha kigaidi cha Daesh amekufa

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: waziri wa mambo ya nje wa Urusi amesema: tunaweza tukasema kwa uhakika mkubwa kuwa kiongozi wa kikundi cha kigaidi cha Daesh “Abubakari Al-Baghdadi nchini Syria tumefanikiwa kumuua.
Waziri huyo aidha ameongeza kusema kuwa tumesema hayo kwa sababu ya kwamba baada ya shambulio liliofanywa na majeshi ya nchi hiyo dhidi ya magaidi hao, ambapo majeshi ya Urusi kwa ripoti ya awali walitangaza kufa kwake kufuatia shambulio lao la anga.
Jeshi hilo lilitangaza kufanya shambulio la anga tarehe 28 mwezi wa tano mwaka huu katika mji wa Raqqah ambapo inasadikiwa kuwa magaidi 330 kikundi cha kigaidi cha Daesh waliuwawa katika shambulio hilo, hivyo kukawa kuna mashaka yakuwa Albaghdadiy ameangamia katika shambulio hilo au hapana.
Katika kauli hiyo iliotolewa na wizara hiyo ni kwamba: kwa mujibu wa ripoti zilio na usahihi Abubakar Al-Baghdad alikuwepo katika kikao kiliokuwa kinafanywa na magaidi hao, ambapo ndege za Urusi zilishambulia magaidi waliokuwa sehemu.
Habari hii imesambazwa katika hali ambayo miaka kadhaa iliopita mara nyingi ilikuwa inatangazwa habari za kuangamia kwa Abubakari Al-baghdadi katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.
Muda mrefu sasa sehemu anayoishi kiongokuzi wa kion gozi wa kikundi cha kigaidi cha Daesh, pamoja yakuwa baadhi ya mida husemwa kuwa alikuwa katika mji wa Musol kabla ya majeshi ya Iraq kuanza mashambulizi ya kuukomboa mji huo mnamo mwezi Oktoba mwaka jana.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky