Waziri wa ulinzi wa Israel: hatuwezi kumtoa madarakani Rais wa Syria

Waziri wa ulinzi wa Israel: hatuwezi kumtoa madarakani Rais wa Syria

Waziri wa Ulinzi wa Israel amesema: ni jambo lisilowezekana kwa rais wa Syria kubaki katika nafasi yake, ama jambo la kumtoa madarakani Rais huyo, ni suala ambalo sisi halituhusu na halipo mikononi mwetu, kwani hatuna nguvu kubwa ya kufanya hivyo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: waziri wa ulinzi wa Israel amebainisha kuwa; Bashar Al-Assad ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Syria anapaswa kutolewa katika nafasi hiyo, ama sisi hatuwezi kufanya jambo hilo.
“Avigdor Lieberman” waziri wa masuala ya ulinzi na usalama wa Israel ameyasema hayo alipokuwa katika mahojiano na Telivishen namba 2 ya Israel, alipokuwa akijibu swali linalohusu kuisha kwa vita ya Syria pamoja na kubaki kwa Rais Bashar Al-assad katika nafasi yake akasema: haiwezekani kwa Rais huyo kubaki katika nafasi hiy, ama suala la kumtoa rais huyo hayatuhusu sisi tu, sisi hatuwezo wa kutosha wa kumtoa Rais huyo, na hatutakiwi kujitia wazimu wa kujihisi tunanguvu zaidi katika hilo.
Aidha ameongeza kusema kuwa; changamoto kubwa ambayo ni tishio kwetu kama jeshi la Israel name kama waziri wa ulinzi wa Israel, ni kujitahidi kuzuia kutokea vita inayotarajiwa kutokea hapo baadae, kwa kuzuia kutokea vita hiyo na kuziongoza pande mbili katika kutatua tatizo hilo kwa mazungumzo, huku wakilipa nafasi zaidi suala hilo.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky