Waziri wa vita wa Israel atuma ombi kwa Rais wa Syria

Waziri wa vita wa Israel atuma ombi kwa Rais wa Syria

Waziri wa ulinzi na vita katika utawala haramu wa Israil amesema: tunamuomba Rais wa Syria haraka iwezekanavyo ayafukuze majeshi ya Iran nchini Syria

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: “Avigdor Lieberman” waziri wa vita wa utawala haramu wa Israel amemuomba Rais Bashar Assad ambaye ni Rais wa jamhuri ya Syria kuwa ayaondoshe majeshi ya Iran katiika taifa lake.
Aidha alipokuwa amekwenda kutembelea na kuangalia milima ya Golan, iliokuwa imeshambuliwa na vibaya na majeshi ya Syria (ambapo kwa mtazamo wa Israel wanadai kuwa mashambulio hayo yamefanywa na majeshi ya Iran yaliopo nchini Syria) ambapo waziri huyo amedai kuwa kuwepo kwa majeshi ya Iran nchini Syria, kwa hakika kutaisaidia serikali ya Syria kwa jambo lolote, bali madhara yake ni makubwa zaidi.
Jambo muhimu kiliashiria ni kwamba: majeshi ya Israel mara nyingi zaidi yamefanya mashambulio mara nyingi nchini Syria, ambapo ndio sababu kubwa ya majeshi ya Syria kujibu mashambulio hayo kwa kushambulia makombora hamsini katika maeneo ya utawala haramu wa Israel ya milima ya Golan asubuhi ya Alhamisi ya wiki iliopita.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky