yalipangwa kufanyika mashambulio matatu katika mji wa Teheran

yalipangwa kufanyika mashambulio matatu katika mji wa Teheran

Kiongozi mkuu wa kupambana na magaidi katika wizara ya ulinzi ametangaza kuwa: asubuhi ya Jumanne timu kadhaa ya magaidi wa Daesh wamefanya shambulio la kigaidi katika mji wa Teheran ambapo mmoja kati yao alikamtwa kabla ya kufanya shambulio lolote

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kiongozi mkuu wa masuala ya kukabiliana na ugaidi katika wizara ya Ulinzi nchini Iran, ametangaza kuwa mashambulizi matatu yalipangwa kufanywa katika mji mkuu wa Teheran.
Aidha kiongozi huyo wa kupambana na magaidi katika wizara ya ulinzi ametangaza kuwa: asubuhi ya Jumanne timu kadhaa ya magaidi wa Daesh wamefanya shambulio la kigaidi katika mji wa Teheran ambapo mmoja kati yao alikamtwa kabla ya kufanya shambulio lolote.
Kiongozi huyo amebainisha kuwa vikundi viwili vya magaidi hao, kimoja kilishambulia sehemu aliokuwa amezikwa Imam Khomeini ambaye ni msimamizi wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran, na kikundi kingine kilishambulia jengo la bunge la Iran, ambapo mmoja kati walishambulia katika Kaburi la Imam aliuwawa kwa risasi za majeshi ya Iran kabla yakufanya tukio lolote na mwengine alijiripua kwa bomu aliokuwa amelivaa.
Kiongozi huyo ametangaza kuwa timu nyingine ya magaidi walipanga kufanya mashambulizi ya klgaidi katika midani ya Baharestani, ambapo walikuwa walikuwa wameanza kurusha risasi wananchi wanaokwenda katika jengo la ofisi za  la nchi hiyo na mwisho wake walitekwa na majeshi ya usalama wa nchi hiyo.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky