Zaidi ya magaidi 80 wa Daesh waangamia kwa muda siku 20

Zaidi ya magaidi 80 wa Daesh waangamia kwa muda siku 20

Kamanda wa mashambulizi dhidi ya magaidi wa Daesh katika majeshi ya kujitolea wananchi nchini Iraq ametangaza kuwa: kufuatia mashmabulizi makali yaliotokea kati yao na kikundi cha kigaidi cha Daesh, wamefanikiwa kuwaangamiza magaidi 80 wa kikundi cha kigaidi cha Daesh ndani ya muda wa siku 20

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Kamanda wa mashambulizi ya dhidi ya magaidi wa Daesh katika majeshi ya kujitolea nchini Iraq ametangaza kuwa, kufuatia mashmabulizi makali yaliotokea kati yao na kikundi cha kigaidi cha Daesh, wamefanikiwa kuwaangamiza magaidi 80 wa kikundi hicho ndani ya muda wa siku 20.
Hayo yamesemwa na Abuhasam As-sahlaniy na kuongeza kubainisha kuwa: kufuatia mashambulizi ya kijeshi ya kikundi cha majeshi ya kujitolea yakishirikia na majeshi ya usalama ya nchini hiyo, ambapo wameangamia magaidi zaidi ya 80 katika mashambulizi ya siku iliopita katika mkoa wa Kirkuk.
Aidha katika mashambulizi hayo wamegundua ghala kadhaa za silaha na vifaa vya miripuko ambavyo vilikuwa wakitumia vikundi hivyo vya kigaidi, inasemekana kwamba majeshi ya uslama ya Iraq yakishirikiana na majeshi ya kujitolea wananchi, wamefanya mashambulizi ya kusafisha mkoa wa Kirkuk kutokana na mabaki ya magaidi wa kikundi cha kigaidi cha Daesh katika maeneo mbalimbali ya maficho ya magaidi hao na kufanikiwa kuwaangamiza wengine kadhaa kuwatia mbaloni.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky