Zaidi ya wabunge 100 wa Uingereza wakemea makala ya kudhalilisha Uislamu

Zaidi ya wabunge 100 wa Uingereza wakemea makala ya kudhalilisha Uislamu

Wabunge zaidi ya 100 wa Bunge la Uingereza kutoka vyama na vikundi mbalimbali vya kisiasa, wamesambaza barua inayokemea makala iliochapishwa na gazeti la The Sun inayo dhalilisha Uislamu

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: wabunge 107 wa Bunge la Uingereza wakitoka katika vyama na vikundi mbalimbali vya kisiasa kwa pamoja wameandika barua dhidi ya gazeti la The Sun, barua ambayo inakemea vikali makala iliochapishwa na gazeti hilo inayo dhalilisha Waislamu nchini humo.
Wabunge kutoka chama cha Democratic, chama cha Green Party, chama cha Liberal, Conservative na Labour, vimekemea vikali makala ilioandikwa iliokuwa na Anuani ya “matatizo ya Waislamu” iliochapishwa na gazeti la The Sun, huku wabunge hao wakionyesha kuunga mkono Jamii ya Waislamu wa nchi hiyo.
Makala hiyo imeashiria baadhi ya matukio maovu wanayofanya baadhi ya vijana wa Kiislamu nchini humo, huku ikieleza kuwa Waislamu nchini humo ndio tatizo kubwa kwa sasa.
Katika barua ilioandikwa na wabunge hao, imeashiriwa kuwa: kitendo cha kuandika makala hiyo ni kosa kubwa lenye hatari nchini humo, jambo ambalo linapaswa kupingwa na kila mtu, huku wakisisitiza kuwa katika karne hii ya 21 A.D. kuandikwa makala kama hiyo na kuchapishwa katika gazeti la serikali ya nchi hiyo ikiwa ni dhidi ya wananchi wachache wanaoishi katika taifa hilo ni jambo la kusitisha na litia aibu.
Aidha katika barua hiyo imeashiria suala la kuenea kutangazwa vibaya waislamu na uislamu katika vyombo vya habari vya nchi za Ulaya huku wakisisitiza kuwa watu hivi sasa wanafahamu kuwa vyombo vya habari hivyo vinalengogani la kusambaza habari hizo ziliokuwa dhidi ya Waislamu na Uislamu, ambapo ukuza hali ya uadui dhidi ya waislamu katika jamii.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky