Zarifu: makubaliano ya Nyuklia bado yataendelea kubaki katika nafasi yake

Zarifu: makubaliano ya Nyuklia bado yataendelea kubaki katika nafasi yake

Muhammad Javad Zarif ameyasema hayo baada ya kuisha kikao cha kikumbuka Afrika mjini Teheran na kusisitiza kuwa makubalaino ya mpango wa Nyuklia wa Iran utaendelea kushika nafasi yake bila ya kuteteleka

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Muhammad Javad Zarif, waziri wa mambo ya nje nchini Iran ameshiriki sherehe ya siku ya Afrika iliofanyika mjini Teheran, mji mkuu wa Iran.
Aidha amesema alipokuwa na waandishi wa habari baada ya kuisha kwa sherehe hizo amesema: makubaliano ya mpango wa Nyuklia wa Iran utaendelea kubaki katika nafasi yake bila ya kuteteleka kwa lolote.
Pia alishiria kuendelea kwa mazungumzo na umoja wa Ulaya na nchi zingine ziliobaki katika kuhifadhi makubaliano hayo amesema: bado tunaendelea kufanya mazungumzo na Umoja wa ulaya na wajumbe wawili wa makubaliano hayo, ili kujua wapi tutafikia katika malengo ya makubaliano hayo.
Waziri wa mambo wa Iran ameendelea kusema kuwa, mpaka sasa tufanya mazungumzo na wajumbe waliobaki katika makubaliano hayo, mazungumzo ambayo tumeshafika katika hatua nzuri na tutaenedelea mazungumzo hayo mpaka tufike mwisho wake.
Mwisho alimalizia kusema na kuashiria fungamano zuri liliopo kati ya Iran na Afrika toka mwanzo wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran, huku akiashiria kuwafungamano la Iran na nchio za Afrika lipo katika  msingi wa kufaika kwa pande zote mbili katika sekta mbalimbali.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky