Binti na mkwe wa Qaradawi wakamatwa nchini Misri

Binti na mkwe wa Qaradawi wakamatwa nchini Misri

Binti ya Yusufu Qaradawi amekamatwa nchini Misri akitihumiwa kuwa amejiunga na kikundi ambacho kifanya harakati zake nchini humo kinyume na sheria na katiba ya nchi hiyo.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA:binti wa shiekh Qardhawi pamoja na mume wa binti huyo ambao ni miongoni mwa viongozi wa chama cha Alwasat wamekamatwa nchini Misri.
Shirika la habari la (youm7) limetangaza katika ripoti yake kuwa watu hao wawili wamekamatwa kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi kwa muda wa siku 15, ambapo watahojiwa kuhusu kuhusika kwao na faili namba 316 la mwaka 2017, kwa maana watuhumiwa hao wanatuhuma ya kujiunga na kikundi kinachofanya shughuli zake kinyume na katiba ya nchi hiyo.
Kwa mujibu wa ripoti hii faili namba 316 pia linawahusu baadhi ya viongozi wa kikundi kilicho sambaratika cha Muslim Brotherhood (udugu wa kiislamu) ikiwemo rais wa Misri alionguliwa Muhamma Mursiy.
Shirika la habari la Youm7 halijataja jina la binti wa Qardhawi ambaye amekamatwa, pamoja jina la mume wake limetajwa kuwa ni Hasam Khalf ambaye ni katika viongozi wa chama cha Alwasat nchini humo.
Yusufu Qardhawi ni Mufti wa Misri aliokuwa na umri wa miaka 90 ambaye ni kiongozi wa kikundi cha kiislamu cha Muslim Brotherhood (Udugu wa Kiislamu) ambapo kuanzia mwaka 1961 mpaka sasa anaishi nchini Qatar.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky