Kamanda wa kikundi cha Daesh aangamizwa kusini mwa Libya

Kamanda wa kikundi cha Daesh aangamizwa kusini mwa Libya

“Abubakari Ashishaniy” ambaye ni katika makamanda wa kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Libya ameangamia kufuatia mapambano makali yaliotokea katika ya kikundi hicho na majeshi ya usalama ya Libya sehemu ya kaskazini ya magharibi ya kisima chama mafuta (Asimaha) kusini mwa nchini hiyo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: habari za kuangamia kwa kamanda mwingine wa Daesh nchini Libya zatangazwa nchini humo.
“Abubakari Ashishaniy” miongoni mwa makamanda wa kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Libya ameangamia kufuatia mashambulio yaliotokea kati ya kikundi hicho na majeshi ya Usalama ya Libya sehemu ya kaskazini ya magharibi ya kisima chama mafuta (Asimaha) kusini mwa nchini hiyo.
Kamanda huyo ameangamia pamoja na magaidi wengine wawili wa kikundi hicho, ambapo miili ya magaidi hao ipo chini ya majeshi ya uslama wa nchi hiyo.
Katika miaka ya hivi karibuni kikundi cha kigaidi cha Daesh kilianza harakati zake za kigaidi nchini Libya na kufanikiwa kuiteka miji kadhaa nchini humo, ama mwishoni miji yote iliokuwa imetekwa na kikundi hicho mpaka sasa imesharudi mikononi mwa majeshi ya Libya.
Kikundi cha kigaidi cha Daesh katika miaka ya hivi karibuni kilianza harakati zake katika mataifa ya Kiafrika kama vile Misri, Libya na Tunisia na kimefanya matukio mbalimbali ya kigaidi katika mataifa hayo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky