Kamanda wa magaidi wa Daesh nchini Libya akamatwa

 Kamanda wa magaidi wa Daesh nchini Libya akamatwa

Majeshi ya Libya yametangaza kumkamata Hishamu Ashmawiy ambaye ni kamanda muhimu wa kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Libya

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: ofisi ya vyombo vya habari katika makao makuu ya majeshi ya Libya imetangaza kuwa majeshi ya ulinzi na usalama yamefanikiwa kumkamata Hishamu Ashmawiy ambaye alikuwa katika viongozi wa zamani wa majeshi ya Misri, ambaye kwa sasa ni katika makamanda muhimu wa kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Libya.
Aidha Hishamu Ashmawiy amekamatwa sehemu ya Al-mughar katika mji wa Danah akiwa katika hali ambayo amejifunga mkanda wa mambomu kwaajili ya kujiripua, ambapo alifanya juhudi ya kutaka kujiripua, ama utaalamu wa wanajeshi wa Libya ulisababisha kushindikana kuripuka kwa mabomu hayo.
Baada ya kukamatwa kwa gaidi huyo, jeshi la Misri limeitaka Misri kumkabidhi gaidi huyo katika utawala wa Misri ili akahukumiwe nchini humo, kwa upande mwingini majeshi ya Libya pia yamefanikiwa kumkamata mke wa gaidi mmoja hatari mwenye jina (Omari Refai Sururu) pamoja na watuto wake nchini Libya.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky