Kikundi cha kigaidi cha Boko Haram chateka mabinti 110 nchini Nigeria

Kikundi cha kigaidi cha Boko Haram chateka mabinti 110 nchini Nigeria

Hilo limetokea kufuatia shambulizi la kigaidi liliofanywa na kikundi cha kigaidi cha Boko Haram katika shule moja iliopo kaskazini mwa mashariki mwa Nigeria na kupelekea kupotea kwa mabinti 110 wanaosoma katika shule hiyo

Shirika la habari AhlulaBayt (a.s) ABNA: wizara ya ulinzi na usalama nchini Nigeria imetangaza kuwa, kufuatia shambulio lilifanywa na kikundi cha kigaidi cha Boko Haram katika shule mmoja iliopo kaskazini mwa nchini na kupelekea kupotea kwa mabinti 110 waliokuwa wakisoma katika shule hiyo.
Kikundi cha kigaidi cha Boko Haram ni katika vikundi vikubwa vinavyoteka watu nchini Nigeria ambapo kilianza kufanya uharamia huo kuanzia mwaka 2014 nchini humo, alkadhalika kikundi cha kigaidi cha Boko Haram kabla ya tukio kilishakuwa kimewateka wasichana zaidi ya 270 wanaosoma katika mashule mbalimbali katika mji wa Jiboki.
Inasemekana kuwa kikundi cha kigaidi cha Boko Haram mpaka sasa ni miaka 9 kinapambana na serikali ya Nigeria na mpaka sasa imeshawateka wanawake na watoto, baadhi ya waliotekwa walirudi makao baada ya kutoa fidia ya pesa kwa kikundi hicho.
Miongoni mwa malengo ya kikundi hicho cha kigaidi kushambulia vituo vya mafunzo ni madai yao kuwa masomo ya sasa kwa wanawake ni sababu ya kuwafanya wanawake hao kujifunza tamaduni za kimagharibi ambazo ni ziko kinyume na mafunzo ya kiislamu, ambapo kikundi hicho kwa muda wa miaka 9 wameuwa wanafunzi wakike 300 na kuharibu shule zaidi ya 400 nchini humo.    
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky