Magaid 20 waangamia kufuatia shambulio la majeshi ya Misri

Magaid 20 waangamia kufuatia shambulio la majeshi ya Misri

Majeshi ya Misri yamefanikiwa kuwaangamiza magaidi 20 katika jangwa la Sinai nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kamanda mkuu wa majeshi ya Misri ametoa kauli na kutangaza kuwaangamiza magaidi 20, alkadhalika wamegundua sehemu 18 ziliokuwa kwaajili ya kujificha katika sehemu hiyo nazo ziliharibiwa na majeshi hayo, huku wakigundua ghala la silaha zao na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa 81 wanaodaiwa kuhusika na mashambulizi ya kigaidi katika sehemu mbalimbali.
Kwa upande mwingine inasemekana kuwa, majeshi ya Misri kufuatia mashambulizi walioyafanya katika jangwa la Sinai, imepelekea kuangamiza magari 39 ya kubeba silaha na kusambaratisha vifaa vingine vya kivita.
Majeshi ya Misri toka mwaka uliopita yalianza mashambulizi makubwa dhidi ya vikundi vya kigaidi katika jangwa la Sinai, ambapo Jangwa la Sinai kuanzia mwaka 2011 kumeonekana kukosa amani na utulivyo ambapo kulitokea vikundi vya kigaidi viliokuwa na mafungamano na kikundi cha kigaidi cha Daesh na kufanya mauji ya kikatiliu katika sehemu hizo.
Majeshi ya uslama ya Misri mpaka sasa kimefanya mashambulizi makubwa dhidi ya vikundi vya kigaidi katika jangwa la Sinai, lakini ripoti bado zinaonyesha kuwa vikundi vya kigaidi vinaendelea kufanya mauaji katika sehemu hizo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky