Magaidi 5 waangamia katika shambulizi la majeshi ya Misri nchini humo

Magaidi 5 waangamia katika shambulizi la majeshi ya Misri nchini humo

Majeshi ya Misri yameshambulia sehemu moja ya maficho ya vikundi vya kigaidi, maficho ambayo yaliokuwa chini ya ardhi waliokuwa wanajificha magaidi ya Daesh katika jangwa la Sinaa nakusababisha kuangamia kwa magaidi watano wa kikundi hicho

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: habari za kuangamia kwa magaidi watano nchini Misri zimesambaa katika vyombo vya habari vya nchi hiyo.

Majeshi ya Misri yameshambulia sehemu moja ya maficho yao yaliokuwa chini ya ardhi waliokuwa wanajificha magaidi ya Daesh katika jangwa la Sinaa na kupelekea kuangamia kwa magaidi watano wa kikundi hicho.

Aidha majeshi hayo pia yamewakamata magaidi watatu wakiwa katika magari mawili katika sehemu ya jangwa hilo nchini humo.

Majeshi ya Misri yalifanya mashambulizi hayo makubwa kwaajili ya kuzikomboa barabara na ziliopo katika jangwa la Sinaa kutoka mikononi mwa kikundi cha kigaidi cha Daesh.

Jangwa la Sinaa toka miaka ya hivi karibuni kumekuwa kukionekana kutokea mashambulizi ya kikundi cha kigaidi cha Ansarul Baitulmaqdas, ambapo kikundi hicho kiliamua kujiunga na kikundi cha kigaidi cha Daesh, hivyo kikundi hicho kuwa tawi la kikundi cha kigaidi cha Daesh mnamo mwaka 2014 nchini humo.

Vikundi vya kigaidi nchini Misri hivi karibuni vilianza kufanya vitendo vya kigaidi nchini humo ambaye vimepelekea kuuwawa kwa mamia ya ya wananchi na wanajeshi wa nchi hiyo na wengine wengi kujeruhiwa.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky