Magaidi 52 wauliwa katika mashambulizi ya majeshi ya Misri

Magaidi 52 wauliwa katika mashambulizi ya majeshi ya Misri

Kamanda mkuu wa majeshi ya Misri amesema katika kauli yake kwamba wamefanikiwa kuwaangamiza magaidi zaidi ya 52 katika mashambulizi yaliofanywa na majeshi yake katika Jangwa la Sinai.

Shirika la habari AhlulByat (a.s) ABNA: kamanda mkuu wa majeshi ya Misri katika kauli yake kunako mashambulizi yanayoendelea nchini humo dhidi ya vikundi vya kigaidi, amesisitiza na kutangaza kuwaangamiza magaidi 52 katika jangwa la Sinai.
Katika ujumbe wake huo amebainisha kuwa, katika mashambulio yaliofanywa na majeshi hayo magaidi 52 wameangamia miongoni mwao 26 ni kutoka katika kikundi cha magaidi hatari zaidi, kadhalika wamefanikiwa kugundua maficho saba na kusambaratisha gari 28 za kkivita waliokuwa nazo magaidi hao.
Aidha wamekamata bunduki 10 nzito za kisasa pikipiki 52, vifaa vya kutengeza mripuko TNT, mabomu ya kutengeza kwa mikono na vifaa vingine vya kivita walivyo viteka katika mashambulizi hayo, huku kukitangazwa kuuwawa kwa wanajeshi 3 katika mashambulizi hayo.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky