Magaidi 8 waangamia kufuatia mapingano kati yao na majeshi ya Misri

Magaidi 8 waangamia kufuatia mapingano kati yao na majeshi ya Misri

Hayo yamesemwa na (Thamir Ar-rifai) msemaji wa majeshi ya ulinzi ya Misri na kutangaza kuwa magaidi wanane wa kikundi cha kigaidi wameangamia katika sehemu ya Sinai baada ya mapambano makali na majeshi ya nchi hiyo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: habari za kuangamia kwa magaidi wanane nchini Misri zasambazwa katika vyomo vya habari, msemaji mkuu wa majeshi ya Misri amesema kuwa majeshi ya Misri yameangamiza magaidi wa wanane katika maeneo ya jangwa la Sinai.
Kwa mujiu wa ripoti hii majeshi ya Misri yakishirikiana na majeshi ya anga ya nchi hiyo, yamefanikiwa kuwaagamiza magaid wanane huko wakimteka gaidi mmoja, huku akisisitiza katika mashambulizi hayo majeshi yamefanikiwa kugundua maficho 8 ya vikundi hivyo na kukuta idadi kubwa ya silaha na mabomu.
Miaka dhaa sasa vikundi vya kigaidi nchini vimekuwa vikifanya matukio ya kigaidi katika sehemu mbalimbali nchini humo jambo liliopelekea kuuwawa mamia ya wanajeshi na wananchi wa nchi hiyo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky