Magaidi wa Misri washambulia majeshi ya Misri katika jangwa la Sinai

 Magaidi wa Misri washambulia majeshi ya Misri katika jangwa la Sinai

Habari za hivi punde zinaeleza kuwa magaidi wa Misri wafanya mashambulizi dhidi ya majeshi ya Misri katika jangwa la Sinai na kupelekea kuuwawa kwa mwanajeshi mmoja wa majeshi ya Misri

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kufuatia mripuko wa Bomu la kutengezwa kienyeji ambalo liliripuka mkabala na gari ya majeshi ya Misri katika eneo liliopo karibu na “Jabalul-halali” sehemu ambayo ipo katika ya jangwa la Sinai na kusababisha kuuwawa kiongozi wa kikosi hicho.
Mripuko huo ulisababisha kuuwawa kwa kiongozi wa kikosi hicho cha jeshi la chini namba 19 aliyekuwa na jina “Ahmad Al-jafari”, na kujeruhiwa wengine wengi katika wanajeshi wa Misri.
Shambulio hilo limefanywa katika hali ambayo majeshi ya usalama nchini humo yakisaidiana na majeshi ya Polisi yalikuwa katika mpango wa kufanya shambulio la kijeshi dhidi ya magaidi waliokuwa na silaha waliopo katika jangwa hilo.
Al kadhalika siku kadhaa ziliopita kikundi cha kigaidi cha Daesh kilitangaza kuhusika kwake na shambulio la kigaidi ambao lilifanywa katika kituo cha ukaguzi cha Polisi katika jangwa la Sinai, shambulio ambalo limepelekea kuuwawa na kujeruhiwa wanajeshi 15 nchini humo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky