Magaidi wanne waangamia nchini Misri

Magaidi wanne waangamia nchini Misri

majeshi bya ulinzi na usalama nchini Misri asubuhi ya leo yamefanikiwa kusambaratisha timu moja ya magaidi katika sehemu ya Al-arishi nchini Misri

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: majeshi ya ulinzi na usalama nchini Misri leo asubuhi yamefanikiwa kusambaratisha timu moja ya kigaidi iliopanga kufanya mashambulizi ya kigaidi katika sehemu ya Al-arish nchini humo.
mafanikio hayo yametokea baada ya mapambano mazito kati ya majeshi ya usalama ya Misri na magaidi hao, jambo ambalo limepelekea kuangamia kwa magaidi wanne na wengineo kufanikiwa kukimbia.
katika mapambano hayo majeshi ya Misri pia yamefanikiwa kuzitia mkononi mabomu 10 na silaha zingine ikiwemo Arapiji na baadhi ya vifaa vingine vya kivita, kwa upande mwingine, majeshi ya Misri siku kadhaa ziliopita walifanya mapambano na watu 11 wenye silaha waliokuwa wamejificha katika moja ya Nyumba ziliopo katika sehemu ya Al-arish na kufanikiwa kuwasambaratisha.
Rais wa jamhuri ya Misri toka mwaka jana alitoa tamko la kukabiliana na magaidi na kuanzisha mashambulizi maalumu dhidi ya vikundi vya gidaidi katika jangwa la Sinai, ambapo vyombo vya habari vinaeleza kuwa mpaka sasa magaidi zaidi ya 150 wameangamizwa katika shambulizi mbalimbali yaliofanywa na majeshi ya Misri nchini humo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky